New Page 1

Ndugu wapendwa, ukitaka kuwafahamu Ndugu Wadogo Wakonventuali ni akina nani, nenda hatua kwa hatua na utafurahia kuwa hapa.

Ndugu Wadogo Wakonventuali ni kikundi cha kitawa cha kimataifa. Hapa Kenya, tuko asilimia dogo ya jumuia kubwa duniani iitwayo shirika la Ndugu Wadogo Wakoniventuali, iliyoanzishwa na Mtakatifu Fransisko wa Assisi huko Italia karne ya kumi na tatu. Mwanzo wa shirika ni mnyenyekevu kama huo na mtakatifu Fransisko wa Assisi ameendelea kuvutia wafuasi waaminifu kutoka pande zote za dunia miaka yote. Katika bara la Afrika peke yake, Ndugu Wadogo Wakonventuali wapo nchi sita, Zambia,Ghana, Kenya, Tanzania, Uganda na Burkinafaso.


Hadi leo, tumekuwepo zaidi ya miaka ishirini hapa Kenya. Kuwepo kwetu hapa nchini kulianzia Ruiri-Meru. Misheni yetu hapa Kenya ipo chini ya provinsiali ya mtakatifu Maksimiliano Maria Kolbe huko Gdansk, Poland. Mungu amekuwa mwema kwetu kwa kujibu sala zetu kwa ajili ya miito na kupitia upendo wake, tumeongezeka kwa idadi. Kufikia mwaka wa 2004 shirika letu hapa Kenya liliongezeka kwa idadi kiasi kwamba liliweza kujitegemea tofauti na hapo awali. Sasa tumefikia kiwango cha kuitwa Kastodia (makao makuu ya wakoniventuali hapa kenya) Hatujaongezeka kwa idadi tu bali pia kwa nyumba. Kwa sasa tunazo nyumba tatu; Meru, Nairobi na Limuru ambayo ndiyo makao makuu ya shirika letu hapa nchini. Hivi karibuni tunatarajia kufungua nyumba mbili mpya. South-C-Nairobi na Subukia. Kwa kuwepo kwetu hapa Kenya, tunatumikia watu kwa njia mbali mbali za kitume. Tunafanya kazi kwenye maparokia, nyumba za malezi ya watawa, nyumba za malezi ya kiroho, nyumba ya uchapishaji, Zahanati, nyumba ya watoto yatima na pia uandishi wa jarida la Maria Imakulata.

Tunaishi maisha ya kindugu bila ubaguzi wa rangi, kabila au nchi, tukishiriki upendo wa Mungu kama waenezaji wa maisha ya kiinjili. Mbali na maisha yetu ya kitume, tunawakilisha Yesu mfufuka kwa maisha yetu. Kama Kristo maskini na mnyenyekevu, kama wana wa Fransisko, lengo letu ni kuwa karibu na watu wa Mungu, tukieneza upendo wake kwa wale wote tunaotumikia



Tunatimiza amri ya Kristo, ambaye kwa neno na matendo, alifunza wanafunzi wake kusali kila wakati. Kwa kumpenda Kristo, aliye uzuri mkuu zaidi, sisi watawa, tukiongozwa na mfano na maneno ya baba yetu wa kiserafi, kuinua roho zetu kwa Mungu, ambaye, ‘alituumba kuwa wanadamu kwa mfano wa Mwanaye Yesu Kristo na kwa roho kufanana naye’, na kuomba kwa baba huyo huyo. Kwa hivyo, maisha yetu yamejengwa kwa sala. Kila siku, huanzia kwa kushiriki pamoja katika ibada takatifu ya misa ambapo tunapata nguvu ya kuishi kila siku tukitafakari mafumbo matukufu ya Mwokozi wetu Yesu Kristo na upendo wa mama yetu, Maria Imakulata..

Mtakatifu Fransisko wa Assisi ndiye mlinzi wa Kastodia yetu. Ndiye pia mwanzilishi wetu. Kwa maisha yake matakatifu, ametuvutia kuishi maisha ya kitakatifu tukifuata nyayo za Kristo . Yaani, Kuishi injili yake Kristo kwa utii, bila chochote na kwa useja. Hivi ndivyo alivyoandika katika kanuni ya maisha. Haya ndiyo maisha yetu.



Bwana akubariki na akulinde
Bwana akuangazie nuru ya uso wake, na kukufadhili;
Bwana akuinulie uso wake, na akupe amani.
(Numbers 6, 24-26)

Cophyright ofmconv.Kenya 2005-2008 created by W.Ulman - Admin Panel - Mail: LogIn


    kiswahili po polsku


   .