Subukia ipo kilometa mia mbili na kumi kutoka Nairobi katika bonde la ufa, jimbo la Nakuru. Cardinal Michael Otunga ndiye alitoa ushauri kuhusu 'Marian shrine' hapa Kenya mwaka wa 2003. Ni yeye pamoja na askofu Ndingi Mwana 'a Nzeki ambaye kwa wakati huo alikuwa askofu wa jimbo la Nakuru. Walipewa jukumu la kutatufa mahali panapofaa. Cardinali ndiye aliyependekeza jina la shrine iitwe "Village of Mary Mother of God".
Hapo mwaka wa 1984, kuna watu walidai kuwa walimwona mwanamke wa kiungwana. Ingawaje kanisa haikudhibitisha rasmi hili tukio, kwa uhakika limesaidia wakristu kufumbua umhimu wa kuwepo kwa Birira Maria mbarikiwa maishani mwao na kufanya hapa mahali panapofaa kwa watu wanaokuja kumtukuza Mungu wakimuuliza Mama Maria awaombee.
Hapo mwaka wa 1988, hii shrine ya "The Village of Mary Mother of God" ilitangazwa rasmi kuwa ya kitaifa. Baada ya mwaka mmoja kuna watu ambao walijitolea kupeana ekari hamsini (50 acres) za shamba na hii ilichangia sana katika upanuzi wa hii shrine. Mnamo tarehe 9/05/1991 misa ya kwanza ilikwisha sherehekewa kama ishara ya kuwashukuru wakaazi wa eneo hilo kwa ukarimu wao. Siku ya 8/012/1991 kuna tukio lililofanyika. Mmoja wa wafanyikazi alipokuwa akikata majani kwa mlima wa hii shrine alipata mahali ambapo palikuwa na unyevu unyevu. Alipochimba mtaro maji yalianza kutiririka chini ya mlima. Jambo la kushangaza ni kwamba, maji haya yanatiririka mpaka wa leo. Kwa wale waliokusudia hili tukio lilikuwa ni ishara kutoka mbinguni maana wakati huo kulikuwa na kiangazi na watu walianza kupigania yale maji.
Tukio la kushangaza lilitokea usiku wa 19/04/1998 ambapo shrine ilichomwa na na sanamu ya Bikira Maria ambayo ilikuwa imetoka Ireland na kichwa chake kikapatikana baadaye kichakani. Kikundi kilichohusika na hicho kitendo walidai ya kuwa wametumwa na mungu ili waharibu hiyo sanamu sababu kwao ilikuwa ni kuabudu sanamu na mungu amewakataza. Baada ya hili tukio msimamizi wa mahali hapa padre John Jones akaanza kuirekebisha shrine na akaoona ni heri alete sanamu nyingine kutoka makao makuu ya msimamizi wa baba mtakatifu Nairobi, baada ya kuidhinishwa na maaskofu, hiyo sanamu ililetwa kwa shrine na ikabarikiwa tarehe 9/12/2000.
Baadaye pakawa mahali mhimu kwa jumuiya ya wakatoriki kutoka pande zote za nchi ili wafanye wakenya wote kuwa familia moja chini ya ulinzi wa Mama Maria. Wakatoriki walijumuika pale kwa ajili ya sacramenti ya kitubia na ibada kuu ya Misa wakiwa wamefunga na kuomba ili amani na umoja idumu nchini. Pia walijumuika pale kwa sababu upendo wao kwa mama Maria na kwa ajili ya mahitaji yao ya kimwili na kiroho.
Padre John Jones aliporudi Ireland kwao, maaskofu walionelea kuwa ni heri shirika liendeleze kazi ya utume mahali hapa. Padre Francis Ruiru kutoka jimbo la Eldoret akawa msimamizi kwa muda. Hapo mwaka wa 2005, chama cha maaskofu kikaonelea ni heri kuwapa Wafransisko jukumu hili. Mnamo tarehe29/08/2005 viongozi wa shirika la wafransiskani waliitikia ombi la maaskofu na tarehe 5/10/2006 wakaanza kazi rasmi.
Watakao tembelea Subukia, watakuta kuna pango - kanisa ndogo yenye sanamu ya Maria, njia ya msalaba, kanisa ndogo ya chemichemi. Msimamizi ambaye ni mfransisko ana mpango wa kuendeleza mahali hapa ili pawe panafaa kwa sala. Kulingana na usaidizi wa kifedha kutoka kwa waumini kutakuwa na kanisa kubwa, nyumba ya kupumzikia kwa wale wanaokuja hapa kwa shrine, nyumba ya masista wa ‘Poor Clares’, kanisa ya sacramenti ya kutubio na kuabudu na ukumbi wa mikutano.
Address:
Conventual Franciscan Friars
Our Lady, Mother of God Friary,
National Shrine of Our Lady, Mother of God
P.O. Box 14250
20100 NAKURU