MTAKATIFU BONAVENTURA, NYUMBA YA MALEZI YA WANAFUNZI NA MAKAO YA MABRUDA NA MAPADRI
Nyumba hii inapatikana katika sehemu ya Nairobi iitwayo Lang’ata karibu na Karen. Kwa sasa nyumba hii inao wanafunzi 26 kutoka nchi mbalimbali kama vile Kenya, Tanzania, Zambia, Ghana na Poland. Kama kituo cha malezi ya Ndugu Wafransisko Wakoniventuali, ni nyumba ya masomo ya dini pia.Nyumba hii ni mshiriki wa chuo cha Tangaza ambacho asili yake ni chuo kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki. Wengi wa ndugu wanafunzi na hasa wanaojiandaa kuwa mapadri katika kanisa katoliki la kiroma, wanasoma Theologia kwa kipindi cha miaka minne. Wapo wengine wanaosoma Falsafa kwenye chuo cha Falsafa ambacho kinamilikiwa na shirika la mitume wa Yesu. Wanafunzi wengine wamesajiliwa katika viwango vya (digrii au diploma) tofauti vya masomo mbalimbali kama; Elimu, mambo ya kiroho, au malezi ya kidini.
Address:
St. Bonaventure Formation House
P. O. Box 24177
00502 NAIROBI
tel. (+254 20) 884481
fax (+254 20) 884208
e-mail: