LIMURU ST

MAKAO YA MAPADRE NA MABRUDA YA MTAKATIFU FRANCISKO, LIMURU

Mji wa Limuru unapatikana kwenye eneo lililoinuka, eneo hili linapakana na mwanzo wa bonde la ufa. Limuru iko karibu kilomita 30 magharibi mwa mji wa Nairobi. Limuru ni mji ambao umeendelea sana kwa sababu ya viwanda mbalimbali kama kiwanda chenye sifa cha kutengeza viatu vya Bata. Idadi ya watu ni kubwa sana kwenye mji wenyewe pamoja na viunga vyake. Ni jambo la muhimu kukumbuka ya kwamba mji huu uko kwenye mwinuko wa vipimo mita 2272 juu ya bahari. Katika mwaka wa 2004 na baada ya maombi rasmi ya Ndugu Wadogo Wakoniventuali hapa Kenya, Provinsi ya Gdansk (Poland) iliamua kuanzisha namna mpya ya uongozi wa kujimudu hapa kenya. Mabadiliko yaliyofanyika ni kwamba Wafransisko Wakoniventuali hapa kenya walipewa jina mpya ‘provincial custody’ yaani makao makuu hapa nchini. Maana yake ni kwamba,Wafransisko hapa Kenya wana mamlaka na uhuru kuliko hapo awali katika kazi za kitume na upanuzi wa shirika hapa nchini na kadhalika. Makao makuu ya uongozi mpya yaani Kastodi, iko Limuru,mahali maamuzi yote yanayohusiana na maisha ya Kifransisko yanafanyika. Mtakatifu Fransisko wa Assisi ni nyumba ya mabruda na mapadri iliyojengwa mnamo mwaka 1992 hapa Limuru. Haya yalifanyika baada ya Wafransisko Wakoniventuali kuitikia mwito wa Kadinali, Maurice Otunga (+2003) ambaye aliwaomba Wafransisko wawahudumie watu wa eneo hilo.


PAROKIA Kiwanda cha kuchapisha vitabu (Kolbe Press) kilianzishwa na Wafransisko Wakoniventuali huko Ruiri-Meru mnamo mwaka 1986. Hiki ndicho kilichokuwa kituo cha kwanza kwa ukubwa katika mkoa wa mashariki. Lengo lake lilikuwa ni kuhubiri injili kwa njia ya uchapishaji. Toleo la kwanza lilikuwa ni jarida la Maria Imakulata, ‘The messenger of Mary Immaculate’ ambalo bado linaendelea kuchapishwa hadi leo. Baadaye kiwanda hicho kilinawiri kiasi kwamba ndicho kilichokuwa maarufu zaidi kwa uchapishaji kanda ya mashariki na katikati mwa Kenya. Uendeshaji wa kiwanda hicho unahitaji kuwasiliana na wateja kila siku, pamoja na vyombo na huduma mbalimbali zinazohitajika kila wakati. Hii ndio sababu ya kuhamishwa kwa kiwanda hicho kutoka Ruiri na kupelekwa Limuru, karibu na Mji mkuu, Nairobi. Wakati huu kiwanda hicho kilikuwa kimenawiri sana tangu kuanzishwa kwake. Tukikumbuka vizuri hapo awali, kiwanda hiki kilianzishwa kama kituo kidogo cha kuchapisha jarida la shujaa imakulata pekee. Wakati wa kuanzishwa kwa kiwanda hicho, hakukuweko na viwanda vingine vya kikatoliki. Mwaka baada ya mwaka, kiwanda hiki kiliendelea na kuimarika zaidi. Wachapishaji wote wa kikatoliki walikuwa wanategemea kiwanda hiki kwa kuchapisha kazi zao lakini kazi iliongezeka sana kiasi kwamba kiwanda hiki hakingeweza kumaliza hiyo kazi. Ilibidi padri John Lempicki (mkurugenzi wa kwanza) aajiri wafanyikazi wanne wa kudumu. Hawa wafanyikazi walishughulikia mashine mbili za kujalidi vitabu, mashine moja ya uchapishaji na mashine nyingine ya ukunjaji. Mashine zingine zilikuwa ndogo na zingeendeshwa na mfanyikazi wa siku (kibarua)

Kwa kulinganisha na viwanda vingine, kiwanda chetu (Kolbe press) ni mojawapo ya viwanda bora zaidi hapa nchini. Hii ni kwa sababu zifuatazo:

1. Vyombo vya kazi: Mashine zilizopo sasa ni za kisasa na hali ya juu sana kinyume na hapo awali. Kunazo mashine mbili (rangi aina moja, rangi aina tatu) za uchapishaji, na mashine zingine zinazotumika kabla na baada ya uchapishaji.
2. Wafanyi kazi: kiwanda chetu kina wataalamu wa uchapishaji wanaotuhakikishia kazi bora.
3. Wateja: Wateja huongezeka siku baada ya siku.kuongezeka kwa wateja ni ishara kuwa wanafurahia huduma zetu.
4. Mapato: Faida ya kazi yetu inaonekana wazi kutokana na kazi bora.



Kiwanda hiki ni matunda ya mtakatifu Maksimiliano Kolbe aliyekuwa Mfransisko wa kwanza katika karne ya ishirini kujihusisha na kazi ya uchapishaji na utumizi wa mitandao (electronic media). Maksimiliano alizaliwa nchini Poland kuelekea mwisho wa karne ya kumi na tisa. Kuanzia karne ya ishirini Maksimiliano aliishi Roma lakini hakufurahishwa na kazi iliyofanywa na freemasons. Mtakatifu Maksimiliano aliunda kikosi cha askari (The militia of Mary Immaculate) ili kupigana na ouvu sanasana freemasons. Hawa walikuwa askari wa Kristo, askari wa kupigana na uovu duniani, baadaye wafuasi wa mtakatifu Maksimiliano wangeendeleza vita hivyo dhidi ya ouvu. Maksimiliano aligudua ya kwamba hangeweza kufikia lengo lake kwa maneno pekee.Hii ndio sababu alionelea vizuri zaidi kuendeleza uandishi/uchapishaji kuhusu kikundi alichoanzisha.Kama raia wa Poland, Mtakatifu Maksimiliano alijiunga na Wafransisko Wakoniventuali na wakaanzisha uchapishaji wao huko Poland.


Bali na kuendesha parokia na kiwanda cha uchapishaji ndugu wadogo wameanzisha pia kituo cha wanawake (St. Antony Women Centre) ambacho lengo lake ni kuwasaidia wasichana kukua kisaikologia na pia kuwapa ujuzi wa ushonaji. Ndugu Wadogo wameanzisha pia jengo mpya (orphanage) ambalo linatumika kwa malezi ya watoto yatima/maskini. Miradi hii inaendelezwa na Masisita wa shirika la Dada wa moyo mtakatifu (Daughters of the Sacred Heart).


Tarehe 6 oktoba 2002, tuliadhimisho miaka10 tangu kuanzishwa kwa parokia yetu hapa Limuru, ilibarikiwa pamoja na kufunguliwa rasmi kwa kituo cha watoto cha mtakatifu Antoni. Tunafuraha sana kwa kukamilisha huo mradi wa watoto. Hio ilikuwa changamoto kubwa sana. Katika eneo la parokia yetu (mitaani) bado wapo watoto wengi ambao bado wanahitaji msaada. Watoto wengi ambao ni yatima hutafuta makao na riziki yao ya kila siku huko mitaani na kwenye kanisa letu. Wanaishi kwenye mitaa wanakaa kwenye vyumba hafifu vilivyoundwa kwa makaratasi. Hali ya watoto ni ya umaskini. Kwa mfano: mtoto mwenye miaka mingi kushinda wote ana miaka kumi na mbili na anatunza ndugu zake wadogo watatu, wanne au watano. Wengine hufa kwa njaa, wengine kwa ukimwi na wengine kwa ukosefu wa matibabu. Hali hiyo ya watoto wa parokia yetu ilikuwa ya kuhuzunisha sana kwetu na ndio maana tuna furaha isiyo na kifani kuona ukamilifu wa nyumba hiyo. Hata ingawa nyumba haina vifaa vyote, tayari tumewakubalia wasichana arobaini lakini nyumba ina nafasi ya watoto themanini na hivi karibuni itakuwa na kiwango hicho cha watoto. Tunafahamu kwamba hatuwezi kuwasaidia wote lakini angalau wale wenye mahitaji ya dharura.

Address:
Conventual Franciscan Friars
P. O. Box 468
00217 LIMURU, Kenya
Tel. (+254 20) 209 12 23
e-mail:

Printing Press
Tel. (+254 20) 201 42 76
Fax (+254 20) 204 88 19
e-mail:

Cophyright ofmconv.Kenya 2005-2008 created by W.Ulman - Admin Panel - Mail: LogIn


    kiswahili po polsku


   .