RUIRI ST MAXIMILIAN FRIARYRuiri Catholic Mission is situated in the Eastern part of Kenya

MAKAO YA MAPADRE NA MABRUDA YA MTAKATIFU MAKSIMILIANI M. KOLBE, RUIRI

Misheni hii inapatikana mashariki mwa Kenya karibu na mji wa Meru (kilomita 14 kutoka Meru) katika jimbo la Meru. Vipimo vya sehemu iliyojengwa misheni hii ni hekta tisa unusu. Misheni hio iko umbali wa kilomita 250 kutoka mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Ndugu Wadogo Wafransisko Wakoniventuali wamekuwepo hapa Kenya tangu mwaka wa 1984.Walifika hapa kenya kufuatia mwaliko wa Askofu mstaafu Silas Njiru wa jimbo la Meru (sasa Askofu emeritus). Baada ya kuwaalika hapa Kenya Ndugu Wadogo Wafransisko Wakoniventuali kutoka Poland, aliwapa ile misheni tarehe 15 Oktoba, 1985. Kuanzia wakati huo Ndugu Wadogo wamekuwa wakiendeleza miradi mbalimbali na kuwahudumia watu kwa njia kadha wa kadha. Majina ya Ndugu Wadogo Wafransisko Wakoniventuali wa kwanza kuja kenya ni: Ndugu Dominic Wasilewski, Ndugu Jan Lempicki na Ndugu Raymond Marszalkowski, wote kutoka nchi ya Poland.

ruiri.jpg (33504 bytes)

Katika misheni yenyewe, kuna parokia, nyumba ya mabruda na mapadri, kituo cha sala, nyumba ya wapostulanti, zahanati na nyumba ya masisita.

Parokia ina vigango 16 ambavyo vinahudumiwa na mapadri walioko pale. Parokia na ukumbi wake zilijengwa katikati ya mwaka 1982-1985 na 1996-1998. Idadi ya wakristo wa parokia hio ni 12,000.

Kituo (nyumba) cha sala kilijengwa katika mwaka wa1991-1994 na kufunguliwa rasmi na Askofu mstaafu Silas Njiru mnamo mwaka wa 1995. kituo hiki hutoa huduma za kiroho kwa wanaozihitaji, inaweza kuwa kama siku ya ukimya inayoandamana na sala au mafungo kwa kipindi fulani.

Kama wanadamu, tunapopata uchovu wa kimwili au kiakili, afya zetu hudhoofika na ndio maana tunahitaji kupumzika vya kutosha ili kudumisha afya bora. Mwanadamu sio mwili na akili pekee, watu wengi husahau ya kwamba roho zetu ambazo zinatuunganisha na muumba wetu ni za muhimu sana. Miili yetu, akili na roho zetu, vyote ni vya kushughulikiwa sawa bila ubaguzi. Ukisahau kitu kimoja kati ya hizo tatu,zile zingine zitaadhiriwa. Katika maisha yetu, tunasumbuka na mambo mengi sana na ndio maana tunahitaji wakati na mahala maalum pa kuimarisha uhusiano wetu na Mungu. Takribani watu 1000 huhudhuria siku za sala na mafungo kwenye kituo hicho. Wengi wao huwa ni mapadri, masisita na mabruda. Mapadri wa jimbo, mashemasi na wanaojiandaa kupata daraja za kanisa huja kwa siku za sala na kutafakari pale. Kunao walei pia ambao wamevutiwa na mradi huo na huwa na siku zao za sala za kibinafsi na hata katika vikundi mbalimbali wakitaka kukutana na mungu kwa kuwa pamoja na mtakatifu Fransisko na mtakatifu Klara.

Kituo hiki huwa na shughuli karibu wakati wote kwa sababu washiriki huja kutoka sehemu mbalimbali za jimbo la Meru. Hawa ni pamoja na mashirika mbalimbali ya mabruda na masisita, mapadri, waseminaristi, na vikundi vya walei. Sisi kama Wafransisko tunajihisi vizuri sana kuandamana na watu katika safari yao ya imani. Sio sisi tunaowaongoza watu hawa bali ni roho mtakatifu mwenyewe,ndiye anayewaongoza na kuwaelekeza. Sisi huwasaidia watu kujua mahali roho mtakatifu anawaongoza. Kazi yetu ni kuhakikisha mazingira bora pamoja na msaada wa kiroho katika kutafuta matakwa ya mungu. Bali na watawa wengi wanaokuja sala/mafungo ya kuhubiriwa au kuelekezwa, tunao pia walei kutoka madhehebu mengine ambao wanapenda kuomba nasi.


Sisi kama Wafransisko tuna moyo wa kuwapokea na kuwakubali watu wa madhehebu mengine.Kwa mfano, mtakatifu Fransisko alienda kuihubiri injili kwa Waislamu. Tunajaribu kuiga mfano wake tunapowakaribisha watu wa madhehebu mengine kwenye nyumba zetu za sala. Wakandidati katika nyumba ya wapostulanti hukaribishwa na kuelezewa kuhusu maisha ya Undugu ya jamii ya Wafransisko Wakoniventuali. Jamii ya wapostulanti inapaswa kunawiri vizuri,hii ndio sababu tunawaamasisha wanafunzi hao kuwa na mashauriano, mijadala, uwazi,makabiliano katika maisha, uhuru na uelewano baina yao. Jamii yetu inanawiri vizuri kwa njia ya sala za kibinafsi na za pamoja. Wakandidati husaidiwa kukomaa katika maisha ya kikristo na kuimarisha uhusiano wao na Yesu Kristo.

Wanafunzi hawa huja kwenye malezi kutoka tamaduni tofauti. Wanajihisi na kuwaza mambo tofauti; wanaona aibu, hawaelewi mambo mengi, hawana ujuzi wa kutosha, wanakosa uhakika, hawajiwezi, wana wasiwasi na kadhalika. Ni wajibu wa mlezi (padri au ndugu) kuwapa malezi bora hao wanafunzi ili waweze kuwa na uhusiano mwema na Kristo pamoja na watu wote.Katika malezi ya wapostulanti, wanafunzi husaidiwa kukua/kuimarika katika mambo mbalimbali katika maisha: kukomaa ki utu, kuelewa uhusiano wa tamaduni za kisekulari na umuhimu wa injili, kuimarika katika maisha ya kitawa/kiroho na maadili, kuzoea maisha ya jamii, kuelewa faida ya karama ya kifransisko.Wanafunzi wenye asili ya kenya na Tanzania huchukua kipindi cha miaka 2 kama wapostulanti. Wanafunzi hawa upata malezi yao ya mwaka wa kwanza kule Ruiri hapa nchini Kenya, kwa mwaka wa pili huenda kwenye nyumba ya malezi kule Arusha,Tanzania.

Kuna Zahanati iliyojengwa katikati ya mwaka 1988-1990 na tangu ilipojengwa imekuwa ikiendeshwa na shirika la Masisita Wamishenari Wafransisko wa Assisi ambao walikuja kenya kutoka zambia mwaka 1990.Watu wengi wa eneo hilo wamepata msaada kutokana na kuwepo kwa hio zahanati. Takribani wagonjwa 2800 huhudumiwa kila mwaka. Baadhi ya magonjwa yanayotibiwa sana ni pamoja na Taifod, malaria, amiba, minyoo na kadhalika. Wanaofanya kazi pale ni, Nesi wawili, Sisita msimamizi na msaidizi wake, msaidizi wa mahabara, msaidizi na mfanyikazi wa mazingira. Kuanzia machi 2004 Masisita Wamishenari Wafransisko wa Assisi waliondoka Ruiri na Masisita wa Felician kuchukua nafasi yao

Address:
Conventual Franciscan Friars
P.O. Box 472
60200 MERU, Kenya
Tel. (+254 20) 209 51 87
E-mail:

tel. Retreat House
Tel. (+254 20) 353 80 67
E-mail:

tel. Postulancy House
Tel. (+254 20) 204 29 45
E-mail:

Nyumba ya masisita ilijengwa katikati ya mwaka wa 1988-1990. Masisita hawa hufanya kazi kwenye zahanati pamoja na kusaidia katika kazi za parokia.Masisita Wamisionari Wafransisko wa Assisi waliishi pale hadi mwaka wa 2002, baadaye iliwabidi waondoke Ruiri ili waweze kuimarisha maisha ya jamii katika nyumba yao ya malezi huko Nairobi.

Nyumba yao pamoja na zahanati zilibakia bila watu/wahudumu hadi viongozi wa Ndugu Wadogo Wafransisko na Masisita wa Felician walipokubaliana kuendeleza kazi hapo.Baadye masisita wapya wa Felician walifika kuanza kazi kwenye zahanati, kufundisha shuleni na kusaidia katika kazi za Parokia.

Address:
Felician Sisters
P.O. Box 1213
60200 MERU, KENYA
tel. (+254 64) 66526

Cophyright ofmconv.Kenya 2005-2008 created by W.Ulman - Admin Panel - Mail: LogIn


    kiswahili po polsku


   .