'Shirika la kwanza lenyewe (la kiume) kama mti uzaao matunda mengi, lilizaa familia mbalimbali za Ndugu Wadogo. Hii ndio sababu inafaa zaidi kwa familia zote zinazomtambua mtakatifu Fransisko kama baba yao wa kiserafi wanajitahidi wakati wote kudumisha mawasiliano ya kidugu ili wakati wowote au mahali popote pale utimilifu wa roho ya kifransisko uweze kunawiri vizuri.'(c.iv.f)
Leo, neno 'Familia ya Wafransisko' inatumika kuelezea mashirika na vikundi mbalimbali ambavyo vinashiriki kuiunda familia hii.
Washiriki wa tawi la kwanza wa shirika la kwanza walijulikana kama 'Ndugu wa jamii' walianzishwa na Mtakatifu Fransisko mwaka wa 1209 na sasa wanaitwa wakoniventuali (OFM Conv). Tawi la pili, kwa kiasili Ndugu wa mgeuzo/kuongoa, iliundwa na jamii nyingi zilizogawanyika kabla na baada ya mgawanyiko wa 1517.Haya matawi ya shirika la kwanza yaliunganishwa pamoja na Baba mtakatifu Leo XIII mnamo mwaka wa 1897 na wakaitwa 'Ndugu Wadogo wa muungano wa Leo' (OFMLeo)
Ili kuepukana na kutoeleweka na kutambulikana, mnamo mwaka 1909, Baba Mtakatifu Pius X alisisitiza jina ‘Ndugu Wadogo wa muungano wa Leo'. Wakapuchini (OFM Cap) walianzishwa mwaka wa 1528 kama tawi la tatu la shirika la kwanza.
Shirika la pili (la kike) lilianzishwa na mtakatifu klara wa Assisi mnamo mwaka 1212. Waklara fukara huishi maisha ya kutafakari katika nyumba zilizotengwa.
Shirika la tatu limeundwa na vikundi viwili vinavyotokana na jamii mbalimbali: shirika la tatu la wasekulari na shirika la tatu la watawa (wanawake na wanaume). Vikundi vyote viwili vinajishughulisha na mahitaji ya jamii.