"Pax et Bonum- amani na salama" Hii ni salamu ya wafransisko ambayo imekuwa ikitumika kwa karne nyingi sana. Tuliipokea kutoka kwake fukara wa Assisi, mtakatifu Fransisko kama rajamu ya maisha yetu ya kifransisko.
Mtakatifu Fransisko alibadilisha kabisa maisha yake wakati alipokutana na Yesu.Fransisko alibadilisha pia uhusiano wake na watu wengine.Akaanza kuiishi maisha ya upendo na jitihada katika kuuhubibiri ufalme wa Mungu. Baadaye katika maisha yake, mtakatifu Fransisko, mungu mwenyewe alimwonyesha salamu hii: Bwana akupe amani! Hii ndio sababu wakatii wote alipowahubiria watu alianza kwa kutamatisha mahubiri yake kwa kutumia salamu hii ya amani.
Salamu hii ya kifransisko imedumu hadi leo. Kama ndugu wa kiroho wa Mtakatifu Fransisko, tunapenda kurudia na kuileta amani katika maisha yetu, ili tuweze kuwa wajumbe wa upendo wa Mungu hapa Duniani. Tunaamini kwamba vurugu na ghadhabu sio suluhisho ya migogoro hapa ulimwenguni. Msamaha pekee, amani na salama ndio chanzo cha uhuru kamili na furaha katika jamii ya wanadamu.