CRUCIFIX OF SAN DAMIANOThe San Damiano Cross is one of the most liked franciscan
symbols
Msalaba Wa Mtakatifu Damiano
Msalaba wa mtakatifu Damiono ni moja wa ishara za kifransisko zinazopendwa sana. Maisha ya mtakatifu Fransisko yalibadilika, wakati alikua akisali chini ya huu msalaba. Picha za msalaba huu ndizo zilimvutia Fransisko ili aweze kuongoka Fransisko pia alisikia sauti ikimwambia aitengeneze upya kanisa la mungu.Haya yalikuwa maandishi yaliyomkumbusha mateso ya Yesu kama yalivyoandikwa na mtakatifu Yohane. Ilikua imewekwa ndani ya kanisa dogo ya mtakatifu Damiano karne moja iliotangulia ili kuonyesha upendo wa Kristo katika mioyo ya watu waliozoea kujifunza imani yao kutokana na rangi, ishara na mifano.
Akiutazama msalaba, Fransisko alikutana na macho ya Yesu msulibiwa na pia Yesu mshindi. Mtakatifu Yohane anatuonyesha kristo aliyetukuzwa. Yesu anatawala matukio yote katika kuteswa kwake, hakuna anayeuchukua uhai wake kwa nguvu, anautoa kwa hiari yake.