Kama mhubiri wa kweli wa kristo, Fransisko alijitia sahihi ya ishara ya msalaba kwa kutumia chaki na hata kwa muundo wa lile vazi (kanzu) lake. Aliuweka msalaba mbele yake nyakati zote, wakati alipokuwa akitafakari mapangoni, alizifunga vijiti viwili pamoja ili aweze kusali mbele ya msalaba: Tunakuabudu ee Yesu na tunakubariki, kwa sababu ya msalaba wako mtakatifu umeuokoa ulimwengu.
Baba mtakatifu, Innocent III alitangaza ya kwamba Fransisko alihitaji kuwekwa sahini ya Tau (kulingana na innocent, hii ilikuwa ishara ya usafi wa kiroho inayowakilishwa na kikosi cha wateule kinachovalishwa mavazi meupe katika kitabu cha ufunuo. (Ufunuo 7:2-14; Ezekieli9:3-6; Kutoka 12:7-14) Wakati Fransisko alisikia hivi alianza kuandika jina lake Kwa ishara ya Tau.
Mtakatifu Fransisko alitia sahini barua na stakabadhi zake zote kwa ishara ya Tau.
Hadi leo ndugu wa kiroho wa mtakatifu Fransisko uvaa Tau shingoni, huitumia hiyo ishara kutia sahihi kwenye stakabadhi mbalimbali na kadhalika.