Kipaji hiki hutegemea vile imani ya kikundi chochote kile inajitokeza kwa matendo. Ndiyo inachokifanya hicho kikundi kitambulike. Kipaji hiki hakibadiliki kiroho lakini hujitokeza katika watu mbalimbali na kazi za kitume kulingana na historia. Kipaji cha wafransisko ni kufuata injili kama alivyofanya mtakatifu Fransisko wa Assisi. Kunazo namna mbalimbali za kufanya hivi;
- kuwa mwaminifu na kushirikiana na Baba Mtakatifu pamoja na uongozi/mamlaka ya kanisa.
- kushiriki katika maisha ya pamoja kama jamaa moja, na kuwa watakatifu.
- kuunda vikao vya uongozi.
- watu kuwa waangalifu katika kutekeleza wajibu wao wa muda.
- kuwa tayari na kuchangamka katika utume, kujiandaa kupambana na mabadiliko na mahitaji ya nyakati tofauti.
- kuhimizana kwa kiwango cha juu cha kuhubiri na kujihusisha na liturujia, wakati wa kutakatifuzwa kupitia nafasi za liturujia kama sanaa na muziki.
- kuanzisha na kuendeleza masomo ya kisayansi katika dini na ulimwengu mzima.