Katika karne za zamani kidogo (middle Ages) watu wengi walivaa nguo za aina moja. Nguo isiyo ya dhamana, kikofia kidogo cha mabegani na kofia (kapuchi) ya kulinda mtu kutokana na mvua.Nguo ingeonyesha umasikini au utajiri wa mtu kulingana na uwezo wake au kiwango chake katika maisha. Kwa sababu nguo za siku hizo hazikua na mifuko, matajiri walivaa mshipi wa ngozi uliofungwa kiunoni, na katika ule mshipi palining’inia mfuko wa pesa, kisu na silaha hatari.
Baada ya kuongoka kwake, Fransisko aliamua kuutupilia mbali mshipi wake na badala yake akajifunga kiunoni kamba ya kawaida kama watu wa kawaida.Baadaye alifunga ule mshipi mafundo matatu kama ukumbusho wa nadhiri au ahadi tatu kwa mungu. Nazi ndizo; ufukara, useja na utii.
Neno ‘habit’ linatokana na neno la kilatini ‘habitus’ambalo maana yake ni ‘kuwa na mtindo fulani katika maisha’. Vazi la nje ni ishara ya uongofu wa kiroho. Kulingana na mila na desturi, vazi hili (habit) linakubalika kama silaha ya wokovu na haki. Katika familia la Wafransisko, vazi (habit) hili huchukuliwa kama vazi la arusi na mazishi. Ni ishara ya umoja na kiunganishi kinachoonekana kati ya ndugu waliotangulia mbinguni na wale ambao bado hawajazaliwa.
Kulingana na historia mbalimbali.,rangi na muundo wa vazi letu zilibadilishwa, kutoka rangi ya udongo ikawa rangi nyeusi kwa wakoniventuali walioko nchi mbalimbali kama Uropa na kazikazini mwa Marekani, rangi ya udongo(kahawia) inavaliwa na wakapuchini na waleonani. Rangi ya kijivu ndiyo inayovaliwa katika sehemu nyingi ulimwenguni, rangi hii inatukumbusha sana juu ya majivu kuliko udongo.