Kama wafransisko, tunashiriki kwa njia tofauti na kwa njia ya pekee kazi ya kanisa, iliyowekwa na Mungu kueneza ufalme wa Kristo kote ulimwenguni kwa utukufu wa Mungu baba yetu. Ili tufanye watu washiriki wa wokovu na kwa ajili yao tuelekeze ulimwengu wote kwa Mungu. Tunafanya juhudi kuishi maisha ya kitume yaliyoelekezwa kwa nia hii.
Kwa kufunga nadhiri, tunajitolea kwa nguvu zetu zote kwa njia ya kipekee kutangaza ujumbe wa Kristo kwa maneno na vitendo, ili neema yake iwafikie watu wa tabaka mbalimbali na tuweze kuwa mashuhuda wa utukufu wake.
Nia yetu kubwa ya kitume ni kuishi maisha ya Kiinjili kati ya watu kwa upendo, umaskini, unyenyekevu na umoja.
Tunajitolea kwa watu wote tukitumikia kanisa na watu wake. Nia yetu ni kutangaza mafumbo ya Kristo na injili yake ya amani, upendo na uongofu, tukiwahimiza watu waishi maisha ya kiinjili. Ni kwa sababu hii hapa nchini Kenya tunajitahidi kuwa karibu na watu wenye mahitaji mbalimbali, wafanyakazi wetu, na wote tunaoishi na tunaoshiriki imani moja nao.
Tunakutana mara kwa mara na wakristo katika jumuia ndogo ndogo za kikristo ambazo zipo katika parokia zetu. Katika mikutano hii, tunawahimiza wakristo wetu kuuliza maswali yanayohusu imani, maisha, mila na desturi na kwa kawaida maswali yote yale ambayo yanahusu maisha yao kama wakristo.
Tunakumbuka hali ya mwanadamu ambayo inahitaji kufanywa upya kila wakati na kuongezewa neema ya Mungu, bila kusahau upendo wa mwokozi wetu ambaye hataki hata mkosefu mmoja afe ila aongoke na aokolewe. Ndugu zetu ambao ni mapadri wanajitolea kwa njia ya kipekee kuonyesha huruma ya Mungu katika sakramenti ya kitubio.
Tukifuata mfano wa mwanzilishi wa shirika letu ambaye aliwatumikia wakoma kwa upendo mwingi, tunawatunza wagonjwa kwa njia ya kipekee kwa kuwatembelea kila mara na kuwapa nafasi ya kupokea sakramenti.
Wakristu wetu wana nafasi ya kushiriki imani yao kikamilifu katika vikundi tofauti ambavyo vipo kwenye kanisa letu. Vikundi hivi vinajali masilahi ya kila mmoja watoto kwa watu wazima. Kila mmoja anaweza kujiunga na kikundi kimpendezacho. Tuko na vikundi kama, Charismatic, Utawa wa tatu (Third Order), Askari wa Maria Imakulata (M.I.), Wafransisko Wadogo (Jufra), Watumishi wa Altare, Kwaya, Muungano wa kina mama (C.W.A.), Muungano wa wanaume (C.M.A.), Sunday school, Vijana wadogo, Vijana, Watetezi wa uhai/maisha, n.k
Our Christians have the opportunity to practice their faith fully in the numerous lay
groups present in all our Parishes. They cater for all the ages and so no one is left out.
Each Christian can join any group, which suits them. We have the Charismatic Renewal
Groups, Secular Franciscans (III Order), Militia of Mary Immaculate (MI), Junior
Franciscans (Jufra), Altar Servants, Choir, Catholic Women Association (C.W.A.), Catholic
Men Association (C.M.A.), Sunday School, Junior Youth, Senior Youth, Pro-lifers, Couples
for Christ, e.t.c.
Tuko na nyumba ya mafungo Ruiri (Immaculate Conception) ambayo inatusaidia kukuza na kuendeleza uhusiano wetu na Mungu. Nyumba hii imefunguliwa kwa watawa wote na walei pia. Imejengwa katika sehemu nzuri ambayo inawapa wanaosali muda mzuri wa kupata utulivu wa maisha na amani ya roho zao.
Ndugu wote wa shirika letu wanaeneza askari wa Maria kwa watawa na walei pia kwa sababu shirika letu linamheshimu Maria kwa njia ya kipekee na pia njia moja murua ya kueneza injili. Njia moja ambayo tunafanya nayo hivi ni kuchapisha jarida la Maria Imakulata (Mesenger of Mary Immaculate).
Tunaeneza injili pia kwa kutumia vyombo vya habari. Tuna kiwanda cha kuchapisha vitabu Limuru (Franciscan Kolbe Press). Kinasaidia kanisa letu hapa Kenya na Africa nzima kueneza habari njema kote kwa kuchapisha vitabu vya mashirika ya kanisa kama vile wanadada wa mtume Paulo na mashirika mengine. Vitabu hivi vinaweza kupatikana katika vyumba vya kuuzia vitabu barani kote.
Tuna chumba cha wasichana waliodhulumiwa na yatima Limuru. Tunawahudumia kina mama pia na miradi ya kujitegemea hapo pia. VileVile tuna zahanati na chumba cha watoto wa mitaani Nairobi. Ni tumaini letu kuwa miradi hii yote itawasaidia watu kuwa raia wema na wakristo wazuri.